Tuesday, September 16, 2014

Je, Njia zako ni sahihi mbele za Mungu?





Ni ukweli kabisa, tena usiopingika, unaishi upendavyo, na hakuna wa kuingilia maisha yako.
Lakini je, wajua hatima ya maisha hayo?
Biblia inasema “iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; lakini mwisho wake ni mautiMithali 16:25
Hapana si hukumu ni ukweli, usipotii na kufuata amri na sheria za Mungu hayo ndio matokeo yake. Basi yakague hayo maisha yako, je? hayavunji na kukiuka maagizo, amri na sheria za Mungu?
Bila shaka utasema ndio! Mungu akusaidie kujitambua uko wapi.
Je, hakuna mambo yamchukizayo Mungu?
 Kama “mambo ya kiburi, ulimi wa uongo, na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; moyo uwazao maw mabya; miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; shahidi wa uwongo asemaye uongo; naye apandaye  mbigu za fitina kati ya ndugu? Tafakari!
Je, hakuna hali ya kuwa rafiki wa dunia?
Soma mstari huu wa biblia kutoka Yakobo 4:4 “enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu?
Je, hujatawaliwa na matendo ya mwili?
Najua utajiuliza ni yapi hayo, ni yafuatayo usipate shida:- uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yafananayo na hayo; ambayo watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu; yaani watakwenda jehanamu ya moto. Sijajitungia hayo, soma Wagalatia 5:19 utaona.
Jiepushe ndugu yangu kuzimu hakufai usiwe mbishi, haya maisha yasikupe kiburi yanapita tu, ipo sehemu uendako kukaa milele, itafute yenye manufaa kwako.Usipoteze wakati amua kubadilika, hujachelewa, mgeukia Mungu na umtafute kwa bidii ili umuone akupe uhakika wa maisha yako ya baadaye. Mpe Yesu maisha yako atakuongoza katika njia ya kumpendeza Mungu kuelekea Paradiso. 

Kwa ushauri, msaada wa Maombi, maswali usisite kunitafuta kupitia simu namba ifuatayo:- 0716 010 920 au Email: hpilula@gmail.com na ukurasa wangu wa facebook (washindi.com) Mungu akubariki