Ni
ukweli kabisa, tena usiopingika, unaishi upendavyo, na hakuna wa kuingilia
maisha yako.
Lakini
je, wajua hatima ya maisha hayo?
Biblia inasema “iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa
mtu; lakini mwisho wake ni mauti” Mithali 16:25
Hapana si hukumu ni
ukweli, usipotii na kufuata amri na sheria za Mungu hayo ndio matokeo yake.
Basi yakague hayo maisha yako, je? hayavunji na kukiuka maagizo, amri na sheria
za Mungu?
Bila shaka utasema
ndio! Mungu
akusaidie kujitambua uko wapi.
Je,
hakuna mambo yamchukizayo Mungu?
Kama “mambo ya
kiburi, ulimi wa uongo, na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; moyo uwazao
maw mabya; miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; shahidi wa uwongo asemaye
uongo; naye apandaye mbigu za fitina
kati ya ndugu? Tafakari!
Je, hakuna hali ya kuwa
rafiki wa dunia?
Soma mstari huu wa
biblia kutoka Yakobo 4:4 “enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia
hujifanya kuwa adui wa Mungu?”
Je,
hujatawaliwa na matendo ya mwili?
Najua
utajiuliza ni yapi hayo, ni yafuatayo usipate shida:- uasherati, uchafu,
ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka,
uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yafananayo na hayo; ambayo watu watendao
mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu; yaani watakwenda jehanamu ya
moto. Sijajitungia hayo, soma Wagalatia 5:19 utaona.
Jiepushe
ndugu yangu kuzimu hakufai usiwe mbishi, haya maisha yasikupe kiburi yanapita
tu, ipo sehemu uendako kukaa milele, itafute yenye manufaa kwako.Usipoteze
wakati amua kubadilika, hujachelewa, mgeukia Mungu na umtafute kwa bidii ili
umuone akupe uhakika wa maisha yako ya baadaye. Mpe Yesu maisha yako
atakuongoza katika njia ya kumpendeza Mungu kuelekea Paradiso.
Kwa ushauri, msaada wa
Maombi, maswali usisite kunitafuta kupitia simu namba ifuatayo:- 0716 010 920
au Email: hpilula@gmail.com na ukurasa wangu wa facebook (washindi.com) Mungu akubariki
|
0 comments:
Post a Comment