Luka 8:14-16
Nazilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote. na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu wa wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumila.
Bwana Yesu asifiwe,
habari niliyokuandikia si mara ya kwanza kuisikia, umeisoma mara nyingi na kuisikia sana tu. Kuna mambo yaliyonitokea mimi nilipokuwa nikitafakari juu ya jamii ya wakristo na hii ndio habari yake:-
Siku moja nilikuwa nasikiliza kipindi cha dini katika redio moja hapa nchini, kilikuwa kinazungumzia habari za kwaresma. Mtumishi wa Mungu aliyekuwa akihutubu alihutubu kwa umahili wote, kisha nikasema utukufu kwa Bwana.
Baada ya hapo maswali kadhaa yakanijia, nami sikuwa na majibu nikamuuliza Roho mtakatifu naye akanipatia majibu.
Swali:
Mbona hawa watu wanafundisha neno kama tunalosoma sisi, mahubiri yaleyale, tatizo ni nini hata sisi tuitwe walokole wao wasiitwe hivyo bali wote ni wakristo?
Majibu kutoka kwa Roho Mtakatifu:
Ni kweli, hao wanaitwa wakristo kwa sababu wanafuata mambo yanayofundishwa na kristo, lakini wao wapo katika mfumo wa dini. Akaniambia dini ni utaratibu alioweka mwanadamu wa kumtafuta Mungu ndio maana makanisani kwao wana liturjia na vitabu vingine vya miongozo ya Ibada; na wokovu ni mpango wa Mungu kutafuta wanadamu, hivyo, waliookoka wametafutwa na Mungu mwenyewe na sio wao waliomtafuta na ibada zao MIMI (Roho mtakatifu) ndiye ninayeziongoza.
Pia, akniambia, wao ni kama mimea iliyopandwa chini ya kivuli cha miti mikubwa, ambayo kwa desturi huwa dhaifu na haiwezi kuzaa matunda. ndipo akanikumbusha kwamba mti wowote usio zaa matunda huukata na kuutupa motoni ukateketezwe.
Ndugu zangu Mungu yupo naye anatafuta watu kwa njinsi hii kwamba uisikie sauti yake ya wito wa wokovu kupitia watumishi wake naye akuweke katika orodha ya watoto wake.
Mungu wa Mbinguni akubariki