Ndugu zangu wapendwa katika Bwana
Bwana Yesu asifiwe! Yesu oyeeh eee!!
Champions Oyeee! Achievers juu!
Who am I?.................. I am the champion.
Sisi tu washindi zaidi ya washindi! Hallelluyaaaa!
Ni mara nyingine tena tumepata fursa ya kuhabarishana mambo machache juu ya ufalme wetu wa Mbinguni ambao mimi Happynus Pilula ni balozi wake mwaminifu hapa duniani kwa wito mkuu nilioitiwa na Bwana wetu Yesu Kristo kama mathayo 22:14 inavyosema "walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache.
Namshukuru Mungu kwa kuniweka katika kundi la wateule yaani wana wa Mungu waliopewa neema ya kufunuliwa mambo ya mbinguni na duniani. Pia wenye haki wake yaani warithi pamoja na mwanae mpendwa Yesu Kristu ambaye ndiye mzaliwa wa kwanza kwa kila kiumbe na aliyepewa kumiliki kila kitu kilichopo hapa duniani. Huo ndio utajiri wangu.
Basi tusome 1 Yohana 2:18-27 ndio kifungu kikuu kitakachotuongoza katika kumchambua mpinga kristo.
18 Watoto, ni wakati wa mwisho;na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwepo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. 20 Nanyi mmepakwa mafuta na yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.21 Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wowote utokao katika hiyo kweli. 22 Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyu ndiye Mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana.23 kila amkanaye Mwana hanaye Baba; amkiriye Mwana naye Baba pia. 24 Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo lnakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya mwana na ndani ya Baba.
Mpinga Kristo ni nani?
Mpinga Kristo ni roho ya uasi ndani ya mtu. Uasi huu unakuwa juu ya jambo lolote lile la kiungu. Roho hii ya uasi kamwe haimkiri Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu
Unawezaje kumtambua mpinga Kristo
- Anatabia za Kiburi
- Anajifanya anajua kila kitu
- Anajihesabia haki; yaani yeye Ni bora mbele za Mungu kuliko wengine, kama ni wokovu basi yeye ndiye aliyeokoka wengine wana mark time, hawajasimama katika wokovu.
- Hapokei ushauri uwao wowote.
Nifanyaje ili kujiepusha naye?
Kabla ya kuepukana nae ni lazima utambue mazingira ya kukutana nae, vilevile utambua kwamba kazi ya huyu mpinga kristo ni kukujengea Imani mpya ndani yako juu ya kile ulichokuwa ukikiamini mwanzo. Imani hii inapatikana kwa kusikia. Kupitia maskio tunasikia, kisha tunatafakari na tunajenga imani ndani yetu. Kwa hiyo, mpinga Kristo anaweza kuwa Mtu yeyote aliye na hiyo roho ya uasi haijarishi ni mtumishi wa Mungu ( mchungaji, Mtume, Nabii, Mwalimu, Mwinjilisti, Askofu) au nani wote inaweza kuwavaa maadamu wametega maskio yao na kufungua mioyo yao na kuhifadhi habari hizo wanazosikia. Kwa hiyo unapowategea maskio yako na kusikiliza habari wanazokuambia juu ya ufalme wa mbinguni na watumishi wa Mungu ambazo kwa uhalisia si kweli, ni fitina tu za kutungwa, ujue tayari hao wametekwa na Ibilisi. Kimbia mara moja na kaa mbali nao kabisa. Hao ni njia ya kukupeleka kuzimu. Mungu mwenyewe amesema "usimguse masihi wangu" wewe ni nani unaye kashfu wenzako? Hiyo ni roho ya Uasi. Roho hii kwa asili innguvu kubwa sana ya kuambukiza kwa wengine. Hawezi kupotea mtu mmoja, lazima aondoke na kundi kubwa.
Pia tumesoma kwamba hawa watu wengine (wapinga Kristo) walikuwa kwetu, inamaana kwamba tulikuwa nao katika huduma zetu lakini wakatoka na kujitenga na kuanza kutunena vibaya pamoja na Kristo Bwana wetu. Ukiona hivyo kaa nao mbali sio wa kwetu hao. Si unajua ule usemi unaosema "kwenye msafara wa mamba hata kenge wapo" ndivyo hata hao. Ndio maana Yohana anatuasa kwamba hawa walifunuliwa tu ili sisi tujue kwamba miongoni mwetu wamo wengi tu wasio wa kwetu yaani wana wa Mungu.
Nitajuaje kama nina elekea kutekwa na roho ya uasi?
Roho ya uasi inapokaribia kuteka nafsi ya mtu, kitu kikubwa inachofanya nikubatirisha ushuhuda wote alionao huyo mtu kuhusu Yesu, Mtumishi wa Mungu Fulani au Huduma fulani au kanisa fulani. Mfano; ulipookoka uliamini kabisa kwamba Yesu anaponya, na wewe ukapokea kabisa huo uponyaji kwa magonjwa sugu yaliyokuwa yanakusibu. Halafu leo unageuka na kusema kanisa Fulani nina mashaka nao, wanatumia nguvu za Nigeria, ni ma- Freemasons wale kuweni makini nao. Wee mwanadamu wee!!!
Angalizo, shika sana kilichokuvuta kwa Kristo yaani huo ushuhuda wako wa awali, huu ndio nguvu yako ya kuendelea kusonga mbele ukichuchumilia ile mede ya thamani. Hakuna jabali litakalo kuangausha ukisimama katika shuhuda za Yesu katika maisha yako.Mungu wa Mbinguni akupe neema ya kumshinda Ibilisi na kuipinga roho hii ya uasi.
Kama hujampa Bwana Yesu Maisha yako na unatamani umpatie leo fanya jambo hili. sema sala
"Bwana Yesu, asante kwa kunifia msalabani ili kulipa deni za dhambi zangu. Naomba unisamehe makosa, uovu na dhambi zote nilizokutendea. Naomba Bwana unisafishe kwa damu yako takatifu ili niwe safi mbele zako nisiye na hatia. Naomba ufute na jina langu katika kile kitabu cha hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima. Ee Bwana nipatie na Roho wako mtakatifu akaniongoze katika maisha yangu haya mapya ili nikuone ukitembea name. Amina"
Kuanzia sasa amini umekwisha okoka. Jambo la muhimu unalotakiwa kulifanya ni kutafuata kanisa linalo hubiri habari za wokovu na ujiunge nao ili upate kufundishwa taratibu za kuishi na Kristo.
Kama ungependa kujiunga nasi, basi tembelea tawi la huduma ya Efatha lililo karibu yako na utapata msaada wa kiroho ili kumjua Kristo. Wasiliana nasi kupitia +255 716 010 920 au email hpilula@yahoo.com