Ndugu yangu mpendwa,
Bwana Yesu, asifiwe!
Kwa nini dhambi umeifanya sehemu ya maisha yako?
Hujui ya kuwa watenda dhambi wote wataishia jehanamu ya moto?
Kwa nini hutaki kuacha dhambi zako?
Ndio, unasema umeokoka mbona uzinzi hauachwi kutajwa kwako, ni wewe ni vidada, wanawake, unabadili kama bodaboda? Madada nao wanabadili wanaume kama ice cream katika mazingira ya joto.
Sikia biblia inasema, mti usiozaa hukatwa na kutupwa motoni, wewe uliumbwa ukiwa mzabibu mwema, imekuwaje leo uwe mzabibu mwitu? Acha mara moja
Kumbuka Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako, alimwaga damu yake ili wewe uwe huru. Mbona hutaki kukubali makosa yako, utasemehewaje usipokubali kosa, kubali kosa na omba msamaha kwa Mungu haraka, neema yake yakutosha.
Achana na mazingira yote yanayokurudisha katika hali ya dhambi. Biblia inasema Mwana akikuweka huru utakuwa huru kweli kweli, kama unaona ipo nguvu ndani yako inayokusukuma kutenda dhambi hizo, nenda kwa Yesu akuweke huru uepukana na adha hizo unazopitia.
Tazama maisha yako hayasongi mbele kila siku uko pale pale, tatizo ni dhambi unazotenda. Kumbuka, Tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi, dhambi huzaa mauti. sasa kutokana na dhambi zako mauti imetokea ndani yako ndio maana hakuna kwako kinachofanikiwa.
Yesu alisema njoni kwangu nyote wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha.
Sema nami maneno haya huku ukiwa umeshika kiuno chako ili kuvunja asili ya nguvu hiyo inayokusukuma kutenda dhambi
"Bwana Yesu nakupenda, wewe ni mzuri ulikufa msalabani kwa ajili yangu. Naomba damu yako ili ya thamani uliyomwaga msalabani inisafishe nakuniweka huru. Mimi (taja jina lako)......... leo nimeamua kuacha dhambi na kukufuata wewew Yesu katika maisha yangu yote. Wewe uliye alpha na Omega. Naomba Roho wako Mtakatifu aniongoze katika maisha yangu yote.
Amina.
Sasa anza maisha yako mapya