Thursday, January 26, 2012

MAMBO MATATU YA MSINGI ILI IMANI YAKO ITHIBITIKE



Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo. Hivyo ili uitwe mtu mwenye imani ya Kristo lazima uwe msikilizaji wa habari za kristo, na zaidi uwe na utayari wa kuyatendea kazi yale uliyosikia ili imani yako iwe hai, kwa sababu imeandikwa Imani bila matendo imekufa. Pia biblia inasema Imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyionekana. Hivyo ili uweze kupokea ahadi za Mungu ni lazima uwe mkamilifu katika imani. Ndio maana anasema mwenye haki wangu ataishi kwa imani, akiwa mwenye moyo wa kusitasita roho yangu haitamfurahia.
Mambo matatu ya msingi ili imani yako ithibitike
  1. Anza kuyawekea msingi yale mambo yote ambayo Mungu anataka uyafanye, yafanye kwa moyo wako wote. Iwe katika moyo mgumu, akili inakataa we fanya. Kufanya hivyo kunaonyesha utii kwa Mungu. Utii ni kufanya vile Mungu anataka na si kama vile wewe unavyotaka.
  2. Jifunze kukiri neno, hata kama mazingira yanakataa. Mfano: usianze kusema mimi siwezi kufanya biashara kwani kila nikianza nashindwa, bali sema utafanya kwani yupo afanyaye.
  • Jifunze kunena mema, na sio kutamka mabaya. Mfano: Ukoo wetu wala sio wa watu wenye akili. Wote tunaishia form 6 tu; au familia yetu sisi wote ni maskini hakuna hata mmoja mwenye baiskeli.
  • Uonyapo kuanzia neno kwanza hata la mwisho onyesha imani.
  • Jitahidi kuongea maneno yanayojenga, mtu wa imani haongei maneno negative.
  1. Jifunze kuwahi kwenye kusanyiko takatifu kila mara,
    usiahirishe kwenda kwenye kusanyiko na watakatifu wenzako kwa sababu zako. Mfano. Kama unafungu la kumi leo, usingoje kutoa kesho toa leo. Kufanya hivyo kunaharakisha mipango ya Mungu kutimia kwako haraka. Wepesi wa kufanya mambo ya Mungu kunafanya yeye Mungu afanye kwa wepesi aliyokuaahidia. Jifunze kubadilika kila inapoitwa leo i.e. jifunze kujikosoa, usingoje watu wakukosoe.
Kama ungependa kuokoka na uone utamu wa Imani hii yetu kwa Mungu katika Kristo Yesu sema sala hii
"Bwana Yesu, asante kwa kunifia msalabani ili kulipa deni za dhambi zangu. Naomba unisamehe makosa, uovu na dhambi zote nilizokutendea. Naomba Bwana unisafishe kwa damu yako takatifu ili niwe safi mbele zako nisiye na hatia. Naomba ufute na jina langu katika kile kitabu cha hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima. Ee Bwana nipatie na Roho wako mtakatifu akaniongoze katika maisha yangu haya mapya ili nikuone ukitembea name. Amina"


Kuanzia sasa amini umekwisha okoka. Jambo la muhimu unalotakiwa kulifanya ni kutafuata kanisa linalo hubiri habari za wokovu na ujiunge nao ili upate kufundishwa taratibu za kuishi na Kristo.
Kama ungependa kujiunga nasi, basi tembelea tawi la huduma ya Efatha lililo karibu yako na utapata msaada wa kiroho ili kumjua Kristo. Wasiliana nasi kupitia +255 716 010 920 au email hpilula@yahoo.com