Tuesday, September 16, 2014

Je, Njia zako ni sahihi mbele za Mungu?





Ni ukweli kabisa, tena usiopingika, unaishi upendavyo, na hakuna wa kuingilia maisha yako.
Lakini je, wajua hatima ya maisha hayo?
Biblia inasema “iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; lakini mwisho wake ni mautiMithali 16:25
Hapana si hukumu ni ukweli, usipotii na kufuata amri na sheria za Mungu hayo ndio matokeo yake. Basi yakague hayo maisha yako, je? hayavunji na kukiuka maagizo, amri na sheria za Mungu?
Bila shaka utasema ndio! Mungu akusaidie kujitambua uko wapi.
Je, hakuna mambo yamchukizayo Mungu?
 Kama “mambo ya kiburi, ulimi wa uongo, na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; moyo uwazao maw mabya; miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; shahidi wa uwongo asemaye uongo; naye apandaye  mbigu za fitina kati ya ndugu? Tafakari!
Je, hakuna hali ya kuwa rafiki wa dunia?
Soma mstari huu wa biblia kutoka Yakobo 4:4 “enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu?
Je, hujatawaliwa na matendo ya mwili?
Najua utajiuliza ni yapi hayo, ni yafuatayo usipate shida:- uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yafananayo na hayo; ambayo watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu; yaani watakwenda jehanamu ya moto. Sijajitungia hayo, soma Wagalatia 5:19 utaona.
Jiepushe ndugu yangu kuzimu hakufai usiwe mbishi, haya maisha yasikupe kiburi yanapita tu, ipo sehemu uendako kukaa milele, itafute yenye manufaa kwako.Usipoteze wakati amua kubadilika, hujachelewa, mgeukia Mungu na umtafute kwa bidii ili umuone akupe uhakika wa maisha yako ya baadaye. Mpe Yesu maisha yako atakuongoza katika njia ya kumpendeza Mungu kuelekea Paradiso. 

Kwa ushauri, msaada wa Maombi, maswali usisite kunitafuta kupitia simu namba ifuatayo:- 0716 010 920 au Email: hpilula@gmail.com na ukurasa wangu wa facebook (washindi.com) Mungu akubariki

 

Tuesday, September 2, 2014

ACHA DHAMBI

Ndugu yangu mpendwa,
Bwana Yesu, asifiwe!

Kwa nini dhambi umeifanya sehemu ya maisha yako?
Hujui ya kuwa watenda dhambi wote wataishia jehanamu ya moto?
Kwa nini hutaki kuacha dhambi zako?
Ndio, unasema umeokoka mbona uzinzi hauachwi kutajwa kwako, ni wewe ni vidada, wanawake, unabadili kama bodaboda? Madada nao wanabadili wanaume kama ice cream katika mazingira ya joto.
Sikia biblia inasema, mti usiozaa hukatwa na kutupwa motoni, wewe uliumbwa ukiwa mzabibu mwema, imekuwaje leo uwe mzabibu mwitu? Acha mara moja
Kumbuka Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako, alimwaga damu yake ili wewe uwe huru. Mbona hutaki kukubali makosa yako, utasemehewaje usipokubali kosa, kubali kosa na omba msamaha kwa Mungu haraka, neema yake yakutosha.
Achana na mazingira yote yanayokurudisha katika hali ya dhambi. Biblia inasema Mwana akikuweka huru utakuwa huru kweli kweli, kama unaona ipo nguvu ndani yako inayokusukuma kutenda dhambi hizo, nenda kwa Yesu akuweke huru uepukana na adha hizo unazopitia. 
Tazama maisha yako hayasongi mbele kila siku uko pale pale, tatizo ni dhambi unazotenda. Kumbuka, Tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi, dhambi huzaa mauti. sasa kutokana na  dhambi zako mauti imetokea ndani yako ndio maana hakuna kwako kinachofanikiwa.

Yesu alisema njoni kwangu nyote wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha.

Sema nami maneno haya huku ukiwa umeshika kiuno chako ili kuvunja asili ya nguvu hiyo inayokusukuma kutenda dhambi
"Bwana Yesu nakupenda, wewe ni mzuri ulikufa msalabani kwa ajili yangu. Naomba damu yako ili ya thamani uliyomwaga msalabani inisafishe nakuniweka huru. Mimi (taja jina lako)......... leo nimeamua kuacha dhambi na kukufuata wewew Yesu katika maisha yangu yote. Wewe uliye alpha na Omega. Naomba Roho wako Mtakatifu aniongoze katika maisha yangu yote.

Amina.

Sasa anza maisha yako mapya

Friday, June 13, 2014

MUNGU NAKUPENDA, WEWE NI MZURI

Na Happynus Pilula
 Hakuna ninacho jivunia duniani zaidi ya kumjua Mungu, Huyo aliye baba yangu, anitulizaye wakati wote na kuniweka katika furaha yake.
Sina BABA mwingine ni wewe pekee pokeaa sifa na utukufu babaaaaaa,..... anipendaye kama wewe ni nani? Asiyetaka nipotee ni nani? Asiyechoshwa na udhaifu wangu ni nani? Anivumiliaye kuwa nitabadilika ni nani? Ni wewe pekee.
Tazama uliko nitoe, tazama nilipo, tazama wanaonizunguka hali zao na mienendo yao, je, leo hii nisingekuwa mmoja wao kama si huruma na upendo wako? Nakushukuru BABA

Wapo mafahari wengi wanapotea, wanashuka kuzimu kila siku. Zaidi ni vijana wenye nguvu wanaenda kuungana na Shetani. Baba naomba rehema zako juu yetu vijana. Tunapotea tunakwisha, tazama tunavyopukutika kwa uzinzi, uasherati, tamaa za mali, ujambazi. Baba nimekujia Wewe uliyetumaini na ngome yangu, msaada wangu wakati wa shida naomba usikie dua yangu na ukatuponye sisi tulio umbwa kwa mfano na sura yako, tuwe wa utukufu kwako, Tusilinajisi jina lako.

Zaidi bwana naomba mstari huu wa Isaya14:9-11 usiwe kimbilio letu vijana. Mahali petu pawe mbinguni paradiso. Tufurahi pamoja na wewe katika karamu ya Mwana kondoo.
"Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako,
Ili kukulaki utakapokuja;
Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako,
Naam, walio wakuu wote wa dunia;
Huwainua wafalme wote wa mataifa,
Watoke katika viti vyao vya enzi.
Hao wote watajibbu na kukuambia,
Je, wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi!
fahari yako imeshushwa hata kuzimu, 
Na sauti ya vinanda vyako;
Funza wametandazwa chini yako,
Na vidudu vinakufunika.

NakupendaYesu, wewe ni Mzuri