Mwanadamu hata lini utafuata njia zako hizo zikupelekazo kuzimu?
Kwa nini kutumainia akili yako na kufuata matakwa ya mwili wako?
Kwanini kuifanya miguu yako myepesi kukimbilia uovu?
Nikuonye mara ngapi ndipo usikie na kuacha uasi wako?
Sikia leo ni kuambialo!
22“Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga?
Na wenye dharau kupenda dharau yao,
Na wapumbavu kuchukia maarifa?
23 Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu………
24 Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa;
Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;
25Bali mmebatilisha shauri langu,
wala hamkutaka maonyo yangu;
26Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu,
Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;
27Hofu yenu ifikapo kama tufani,
Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli,
Dhiki na taabu zitakapowafikia.
28Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika;
Watanitafuta kwa bidii, wasinione.
29Kwa kuwa walichukia maarifa,
Wala hawakuchagua kumcha BWANA.
30Hawakukubali mashauri yangu,
Wakayadharau maonyo yangu yote.
31Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao,
Watashiba mashauri yao wenyewe.
32Maana kurudi nyuma kwa wajinga kutawaua,
Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.
33Bali kila anisikilizaye atakua salama,
Naye atatulia bila kuogopa mabaya.”( Mithali 1:22-33)
Muda ni huu hujachelewa, acha njia zako na umgeukie Mungu. Kwa msaada wa maombi, ushauri, una swali usisite toa maoni yako katika blog hii au piga simu +255 716 010 920, +255 752 813 618, au tuma email: hpilula@yahoo.com or goodnews.forlife@yahoo.com
0 comments:
Post a Comment